Sisi, wanachama wa chama cha kimataifa cha maendeleo ya Kiesperanto, tunatoa tangazo hilo kwa serikali zote, vyombo vyote vya kimataifa na binadamu wote wenye nia njema, tunatangaza nia yetu kuendelea kwa bidii kukidhi madhumuni yaelezwayo hapa chini tukiita kila chama na kila mtu waungane nasi katika juhudi zetu.
Tangu
zaidi ya karne moja Kiesperanto, kilichoanzishwa mnamo 1887 kama
mpango wa lugha kisaidizi katika mawasiliano ya kimataifa na kilichogeuka
upesi kuwa lugha yenye maana nyingi na uhai wa peke yake, ni njia
ya kuunganisha watu kupita migogoro ya kilugha na ya kiutamaduni.
Wakati huo huo madhumuni ya Kiesperanto hayajakosa maana na muhimu.
Wala utumizi wa lugha kadhaa za kitaifa katika dunia nzima wala
maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano, wala ustawi wa mbinu mpya
za fundisho la lugha hazitatekeleza mfumo wa kilugha ulio sawa
na wa kufaa unaotegemea kanuni zifuatazo na tunazozihesabia za
lazima.
DEMOKRASIA
Kila mfumo wa mawasiliano unaowapendelea
watu wachache daima, huku unawalazimisha wengine watoe miaka ya
juhudi ili wapate kiwango cha chini cha umahiri (ufasaha na usahihi)
ni kinyume kabisa cha usawa. Ingawa Kiesperanto, kama lugha yoyote,
si kamilifu, kinapita kabisa kwa usawa lugha zote zitumikazo kwa
mawasiliano popote duniani.
Sisi tunathibitisha kwamba ukosefu
wa usawa wa kilugha unazaa ukosefu wa usawa wa kimawasiliano katika
viwango vyote, pamoja na kiwango cha kimataifa.
Sisi ni ushirikiano unaotaka mawasiliano
yenye usawa.
ELIMU
YA KIMATAIFA
Kila lugha ya kitaifa inaungana na
utamaduni fulani na taifa au mataifa fulani. Kwa mfano, mwanafunzi
anayesoma Kiingereza anafundishwa utamaduni, jiografia na mifumo
ya kisiasa za mataifa yanayotumia Kiingereza, hasa Marekani na
Uingereza. Mwanafunzi anayesoma Kiesperanto anafundishwa kuhusu
dunia bila mipaka, ambapo taifa yo yote si ngeni kwake.
Sisi
tunathibitisha kwamba elimu ikitekelea kwa njia ya lugha yoyote
ya kitaifa imeungana na maoni fulani ya ulimwengu.
Sisi ni ushirikiano unaotaka elimu
ya kimataifa.
MANUFAA
YA KIMAFUNZO
Asilimia chache tu ya wanafunzi wa
lugha ngeni wanafikia umahiri wa lugha lengwa hiyo. Umahiri wa
Kiesperanto unafikiwa hata kwa masomo ya kitabuni. Utafiti umeonyesha
kwamba Kiesperanto inafaa kama andalio la masomo ya lugha zingine.
Tena, kimependekezwa kama sehemu ya maana hasa katika masomo ya
utambuzi wa kilugha.
Sisi
tunathibitisha kwamba matatizo katika ujifunzaji wa lugha za kitaifa
yatakuwa daima kikwazo kwa wanafunzi wengi ambao wangefaidi kutoka
ujuaji wa lugha ya pili.
Sisi ni ushirikiano unaotaka kuendeleza
ujifunzaji halisi wa lugha.
ULUMBI
Jamii ya Kiesperanto karibu haina kifani
kama jamii ieneayo popote duniani: watumizi wake wajua lugha mbili
au zaidi. Kila mwanajamii amejitihadi kujifunza angalau lugha
ngeni moja kufikia kiwango cha kuwasiliana. Nyakati nyingi hicho
kinaelekea kuzipenda na kuzijua lugha nyingi na kwa jumla kupanua
fikira zake mwenyewe.
Sisi
tunathibitisha kwamba watumizi wa kila lugha, kubwa au ndogo,
lazima wawe na nafasi ya kweli ya kusoma lugha ya pili kufikia
kiwango cha juu cha kimawasiliano.
Sisi ni ushirikiano unaotaka kuwapa
wote fursa hiyo.
HAKI
ZA LUGHA
Ugawanyaji wa uwezo usio sawa kati
ya lugha ni chanzo cha mashaka ya kilugha ya daima, au udhalimu
dhahiri wa kilugha, kwa baadhi kubwa ya binadamu. Katika jamii
ya Kiesperanto watumizi wa lugha kubwa na dogo, iliyo au isiyo
rasmi wanakutana katika usawa kwa sababu ya mapatano ya kuridhiana.
Usawa huo wa haki za lugha na madaraka unatoa msingi wa ustawishaji
na uchunguzi wa matatuzi mengine ya utofauti na mpambano wa lugha.
Sisi
tunathibitisha kwamba tofauti kubwa za uwezo baina ya lugha zinadhoofisha
hakika, inayotajwa katika vyombo vingi vya kimataifa, ya usawa
bila kujali lugha.
Sisi ni ushirikiano unaopigania haki
za lugha.
UWINGI
WA LUGHA
Serikali za kitaifa zinaelekea kuhesabia
uwingi mkubwa wa lugha duniani kama kikwazo cha mawasiliano
na maendeleo. Katika jamii ya Kiesperanto, walakini, uwingi
wa lugha unafikirika chanzo thabiti na cha lazima cha ustawishaji.
Kwa sababu hiyo kila lugha, kama viumbehai vyote, asili yake ni
ya thamani na inastahiki ulinzi na msaada.
Sisi tunathibitisha kwamba sera za mawasiliano na maendeleo zisizotegemea heshima na msaada kwa kila lugha zinazihukumu wingi wa lugha za dunia ziuawe.
Sisi ni ushirikiano unaothamini uwingi
wa lugha.
UHURU
WA BINADAMU
Kila lugha inafungua na inafunga watumizi
wake kwa kuwapa ubingwa wa kuwasiliana baina yao lakini inazuia
mawasiliano na wasemaji wa lugha nyingine. Kiesperanto, kilichopangwa
kama njia ya mawasiliano ya watu wote, ni mmojawapo wa mipango
mikubwa inayofaa kwa ukombozi wa binadamu - kinachokusudia kumwezesha
kila raia ashiriki kabisa jamii ya binadamu, akiwa na shina imara
ndani ya utamaduni na lugha yake, lakini asizuiwe nayo.
Sisi
tunathibitisha kwamba bila shaka kutumia lugha za kitaifa tu kunaweka
vikwazo vya uhuru wa kusema, kuwasiliana na kushirikiana.
Sisi ni ushirikiano unaopigania uhuru
wa binadamu.
Praha, Julai 1996
Tafsiri ya Nino Vessella / 7 Julai 1997
Kwa kulingana na Web Counter,
wewe ni msomaji wa .