Karibu!

Heri nyingi kwa Mwaka mpya!

<%=Date()%>
Andika kadi
au
ona ile uliyoipata!

Habari zangu


Matembezi yangu (Tanzania)

Anwani za wavuni ninazopendelea:

Kiesperanto

Ni lugha...
Lugha iliyotungwa kwa kusudi la kurahisisha mawasiliano baina ya watu wa nchi mbalimbali. Matumizi ya miaka mia yamethibitisha bayana kwamba Kiesperanto ni lugha inayoweza kueleza mawazo yote ya kibinadamu.
... ya kimataifa na isiyopendelea mtu,...
Kiesperanto siyo lugha ya kabila wala taifa moja; kwa hiyo haipendelei utamaduni mmoja ambao ungeweza kudhulumu au kudhuru tamaduni nyingine. Kiesperanto ni lugha ya mtu yeyote anayeisema na ni kama daraja kati ya tamaduni.
... ni rahisi!
Sarufi ya Kiesperanto ni rahisi. Kiesperanto kina irabu zile zile za Kiswahili na konsonanti sawa na zile za Kiswahili. Maneno ya Kiesperanto yanaundwa, kama maneno ya Kiswahili, toka kiini kimoja kwa kugeuza kiini chenyewe. Basi, kwa kuwa hiyo ni lugha kwa matumizi ya kimataifa, lugha hiyo haifanani na lugha za Afrika tu, bali pia inafanana na lugha za mabara mengine. Wataalamu wamethibitisha kwamba Kiesperanto ni rahisi kuliko lugha nyingine.

Kwa nini tujifunze Kiesperanto?

Kwanza kabisa kwa maana lugha ya kiingereza si rahisi na haikuenea duniani kama watu wengi wanavyofikiria; lakini sababu nyingine zipo pia:

Kupata marafiki
popote duniani; lugha ya Kiesperanto husemwa na mamia ya watu po pote ulimwenguni ambapo wakaapo watu watakao kuwasiliana na kufahamiana kwa kusudi la kuhifadhi amani na kuleta usalama duniani.
Waesperanto wako huko Misri na Urusi, Malagasi na China, Senegal na Vietnam, Marekani na Hungari, n.k. Inawezekana kusoma magazeti kwa lugha ya kimataifa yanayotolewa mjini Roterdam na Tokyo, Mosko na Hanoi, n.k. Inawezekana kusikia idhaa ya lugha ya kimataifa kupitia vituo vya redio mbalimbali na inawezekana kusoma maandishi ya fasihi mbalimbali toka kila pembe ya dunia.

Kufahamu tamaduni nyingine
Tena mintarafu ya utamaduni, Kiesperanto kimejitokeza kama kiwakilisho cha tamaduni zote vile vile; kwa hiyo hakilazimishi mtu anywe utamaduni mmoja tu, bali kinawezesha mlingano wa tamaduni mbalimbali, na kinawezesha kuchagua ya wema popote yalipo.

Tangazo la Praha

Tujfunze vipi?

Unaweza kujipatia habari nyingine za lugha ya Kiesperanto kutoka kwa:

    Umoja wa Kidunia wa Waesperanto - U.Ki.Wa.
    Universala Esperanto-Asocio - U.E.A.
    Makao Makuu
    Nieuwe Binnenweg 176,
    3015 BJ Rotterdam, Uholanzi.
    <uea@inter.nl.net>
   

unaweza pia kujipatia sarufi hii ya kiesperanto: Nino Vessella, Esperanto, jifunze lugha ya kiesperanto,Rotterdam: 1983, lakini ukitaka kuisoma wavuni piga juu yake!

mwishoni, unaweza kujifunza Kiesperanto kwa njia ya masomo haya kwenye wavu.

Ukihitaji kamusi, tazama hapa: Kamusi ya Kiswahili na Kiesperanto

>> Kwa heri! <<



© Nino Vessella , 1996-.
Diritti riservati. Nessuna parte può essere riprodotta, in qualsiasi forma o mezzo, senza citare la fonte.
Ĉiuj rajtoj rezervitaj. Neniu parto povas esti reproduktita, en kiu ajn formo au per kiu ajn metodo, sen mencii ĉi tiun fonton.
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kunakili sehemu yoyote bila kuitaja asili yake hii.
All rights reserved. No part may be reproduced, in any form or by any means, without mention of this source.

1998 05 23
Wageni kuanzia machi 2006